Lugha Nyingine
Luteni Jenerali wa Jeshi la Russia auawa kwenye mlipuko ndani ya gari mjini Moscow
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 23, 2025
![]() |
| Picha hii iliyopigwa Desemba 22, 2025 ikionyesha eneo la mlipuko wa gari kwenye Mtaa wa Yasenevaya, Kusini mwa Moscow, Russia. (Xinhua/Hao Jianwei) |
MOSCOW - Kamati ya Uchunguzi ya Russia imesema, Luteni Jenerali wa Jeshi la Russia Fanil Sarvarov ameuawa kwenye mlipuko wa bomu ndani ya gari mjini Moscow jana Jumatatu, na kifaa chenye uwezo wa kulipuka kilitegwa chini ya gari lake na kulipuka kwenye Mtaa wa Yasenevaya, Kusini mwa Moscow asubuhi ya siku hiyo.
Kamati hiyo imesema kwamba, Sarvarov ambaye ni Mkuu wa Kurugenzi ya Mafunzo ya Kioperesheni ya Ofisi ya Mnadhimu Mkuu wa Vikosi vya Jeshi la Russia, amefariki kutokana na kujeruhiwa vibaya.
"Uchunguzi umeanzishwa kuhusu mauaji hayo, huku mamlaka zikichunguza sababu mbalimbali zinazowezekana, ikiwa ni pamoja na madai ya kuhusika kwa idara maalum ya Ukraine," kamati hiyo imeeleza.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




