Lugha Nyingine
Misri yaanza kuunganisha tena sehemu za jahazi la farao wa kale kwenye jumba jipya la makumbusho (4)
CAIRO - Misri jana Jumanne ilianza kuunganisha tena sehemu za Jahazi la Jua la pili la Mfalme Khufu wa kale kwenye Jumba la Makumbusho Kuu ya Misri (GEM) lililofunguliwa hivi karibuni, mchakato wa ukarabati unaokadiriwa kuchukua muda wa miaka minne hivi na kufunguliwa kwa watalii kutazama moja kwa moja huko.
Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale wa Misri Sherif Fathy amesema uunganishaji huo wa sehemu za jahazi hilo baada ya kufanya kwa miaka mingi uhifadhi, utunzaji rekodi za nyaraka na uchanganuzi wa 3D wa vipande vya jahazi, akisisitiza umuhimu wake wa mali ya urithi duniani.
Jahazi hili lenye umri wa miaka 4,500, liligunduliwa kwenye sehemu iliyo karibu na Piramidi Kuu, kaburi la Mfalme Khufu, mwaka 1954. Jahazi hilo lina vipande vya mbao vipatavyo 1,650 na lenyewe lina urefu wa mita takriban 42.
"Jahazi la Jua la kwanza la Mfalme Khufu lilipopatikana lilionekana karibu ni la kikamilifu, lakini jahazi la pili, ambalo ni dogo kiasi , lilipopatikana lilionekana kuwa na hali mbaya sana," amesema Mkurugenzi Mtendaji wa GEM Ahmed Ghoneim.
"Ukarabati mbele ya watalii ni jambo ambalo huwezi kuliona katika majumba ya makumbusho kote duniani," Ghoneim amesema, akisisitiza uzoefu wake wa kipekee wa kielimu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




