Lugha Nyingine
Handaki refu zaidi duniani la barabara ya mwendokasi lakamilika (3)
![]() |
| Daraja No. 10 la Qianxia kwenye barabara ya mwendokasi ya Urumqi-Yuli (picha ilipigwa Desemba 20, 2025). (Xinhua/Hu Huhu) |
Handaki la Shengli la Milima Tianshan lina urefu wa kilomita 22.13 ni handaki refu zaidi duniani la barabara ya mwendokasi. Hivi sasa, barabara ya mwendokasi ya Urumqi-Yuli, liliko handaki hilo itazinduliwa rasmi.
Barabara ya mwendokasi ya Urumqi-Yuli, ambayo ni mradi muhimu wa kitaifa, ina urefu wa kilomita 324.7, ambayo mazingira ya ardhi ni yenye utatanishi kando zake mbili. Wajenzi walifanya juhudi kubwa kwenye ujenzi wake katika sehemu za Milima Tianshan, wakiondoa matatizo mengi magumu ya ujenzi wa barabara ambayo yalitokea pia duniani, na kuunganisha mahandaki na madaraja kwa ajili ya kuvuka mabonde makubwa, na ujenzi wa barabara hiyo ulikamilika kwa muda wa miaka mitano.
Baada ya kuzinduliwa kwa barabara hiyo, muda wa usafiri wa kutoka Mji Urumqi hadi Mji Korla wa Xinjiang, China utapunguzwa kuwa saa 3.5 hivi kutoka masaa 7.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




