Bidhaa za Yuan bilioni 1.1 zisizotozwa ushuru zauzwa katika wiki ya kwanza ya uendeshaji maalumu wa forodha kisiwani Hainan (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 26, 2025
Bidhaa za Yuan bilioni 1.1 zisizotozwa ushuru zauzwa katika wiki ya kwanza ya uendeshaji maalumu wa forodha kisiwani Hainan
Wateja wakinunua bidhaa kwenye eneo la kimataifa la maduka yasiyotozwa ushuru la Sanya, Hainan, China. (Xinhua)

Katika wiki ya kwanza ya uendeshaji maalumu wa forodha wa Bandari ya Biashara Huria ya Hainan, manunuzi ya bidhaa zisizotozwa ushuru wakati wa kuondaka kisiwa hicho yalidumisha hali ya kuongezeka, na wimbi la manunuzi lilikuwa katika hali motomoto.

Takwimu za forodha ya Hainan zimeonesha, katika wiki ya kwanza ya uendeshaji maalumu wa forodha wa Hainan (tarehe 18~24, Desemba), forodha hiyo kwa jumla ilikagua manunuzi ya bidhaa za Yuan bilioni 1.1 (takriban dola za kimarekani milioni 156.9) zisizotozwa ushuru wakati wa kuondoka kisiwa. Hayo yameongezeka kwa asilimia 54.9 hivi yakilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha