Ndege ya kujiendesha bila rubani ya Lanying R6000 tiltrotor yakamilisha usafiri wake wa kwanza huko Deyang, China (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 29, 2025
Ndege ya kujiendesha bila rubani ya Lanying R6000 tiltrotor yakamilisha usafiri wake wa kwanza huko Deyang, China
Ndege isiyo na rubani (UAV) ya Lanying R6000 tiltrotor ikipaa katika Mji wa Deyang, Mkoa wa Sichuan, Kusini Magharibi mwa China, Desemba 28, 2025. (Picha/VCG)

Ndege ya Lanying R6000, ndege ya tiltrotor ya kujiendesha yenyewe bila rubani (UAV) yenye uzito wa tani 6 iliyoundwa na Shirika la Ndege la United la China, imekamilisha usafiri wake wa kwanza katika Mji wa Deyang, Mkoa wa Sichuan, Kusini Magharibi mwa China jana Jumapili, ikionesha China imepiga hatua mpya katika tekolojia ya usafiri angani wa kuruka na kutua kwa wima.

Ndege hiyo ya UAV ina uwezo wa kubeba mzigo wa hadi kilo 2,000, ikiwa na kasi ya juu zaidi ya kusafiri kwa kilomita 550 kwa saa na umbali wa kilomita takriban 4,000 na kufikia mwinuko wa hadi mita 7,620.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha