Ujenzi wa mnara mrefu zaidi wa daraja uliojengwa baharini wakamilika katika Zhoushan, Mkoa wa Zhejiang wa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 31, 2025
Ujenzi wa mnara mrefu zaidi wa daraja uliojengwa baharini wakamilika katika Zhoushan, Mkoa wa Zhejiang wa China
Picha iliyopigwa Desemba 30, 2025 ikionyesha kilele cha mnara mkuu No. 5 wa daraja la njia ya reli na barabara la Xihoumen la Zhoushan, Mkoa wa Zhejiang, mashariki mwa China. (Xinhua/Huang Zongzhi)

Ujenzi wa muundo wa juu wa Mnara mkuu No. 5 wa daraja la njia ya reli na barabara la Xihoumen kwenye Reli ya Ningbo-Zhoushan katika Mkoa wa Zhejiang, Mashariki mwa China umekamilika jana Jumanne, na kuufanya kuwa wa kwanza wa aina yake kufikia hatua hiyo kwenye njia nzima ya reli hiyo. Mnara huo wenye urefu wa mita 294, takribani sawa na jengo la ghorofa 100, unaweka rekodi mpya ya dunia ya kuwa mnara mrefu zaidi wa daraja uliojengwa baharini.

Daraja hilo la njia ya reli na barsabara la Xihoumen linatumiwa kwa pamoja na Reli ya Ningbo-Zhoushan na Barabara Kuu ya Ningbo-Zhoushan ili kuweza kuvuka barabara ya majini ya Xihoumen huko Zhoushan.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Renato Lu)

Picha