Treni ya mwendokasi ya Bustani ya Dunia ya Barafu na Theluji ya Harbin yaanza kutoa huduma mkoani Heilongjiang, China (6)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 05, 2026
Treni ya mwendokasi ya Bustani ya Dunia ya Barafu na Theluji ya Harbin yaanza kutoa huduma mkoani Heilongjiang, China
Abiria wakipiga picha ya kundi ndani ya treni ya mwendokasi No. G1276, treni ya kwanza ya mwendokasi ya Bustani ya Dunia ya Barafu na Theluji ya Harbin, Januari 4, 2026. (Xinhua/Zhang Tao)

HARBIN - Treni ya kwanza ya mwendokasi mahsusi ya Bustani ya Dunia ya Barafu na Theluji ya Harbin imefunga safari kutoka Stesheni ya Magharibi ya Harbin katika Mkoa wa Heilongjiang, kaskazini-mashariki mwa China jana Jumapili, ikielekea Mji wa Wuhan katika Mkoa wa Hubei, katikati mwa China.

Ikiwa na mapambo ya kipekee ya ndani na nje ya Bustani ya Dunia ya Barafu na Theluji ya Harbin, treni hiyo ya mwendokasi inatumika kama alama inayotembea ikisaidia kuhimiza uchumi wa barafu na theluji.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha