China yashuhudia idadi inayovunja rekodi ya kampuni za utalii wa barafu na theluji (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 06, 2026
China yashuhudia idadi inayovunja rekodi ya kampuni za utalii wa barafu na theluji
Watu wakitembelea Bustani ya Dunia ya Barafu na Theluji ya Harbin huko Harbin, Mkoa wa Heilongjiang, kaskazini mashariki mwa China, Januari 5, 2026. (Xinhua/Wang Jianwei)

HARBIN – Shughuli za Utalii katika mazingira ya barafu na theluji nchini China zinaingia "kipindi kipya cha ustawi endelevu," ripoti iliyotolewa jana na taasisi ya utalii ya China imesema kuwa, hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2025, idadi ya kampuni zinazoendesha shughuli hizo zimefikia 14,075, ambayo imefikia rikodi mpya katika historia.

Ripoti hiyo, iliyotolewa kwenye Jukwaa la Maendeleo ya Utalii wa Barafu na Theluji 2026 katika Mji wa Harbin kaskazini mashariki mwa China, imesema kiwango hicho kinatokana na kuongezeka kwa bidhaa bunifu za utalii, ikiwa ni pamoja na sanaa za michongo ya barafu, upigaji picha kwenye mazingira ya barafu na theluji, na uzoefu wa safari za utalii zenye mada tofauti katika sehemu mbalimbali nchini China.

Ripoti hiyo inaonyesha kwamba maeneo maarufu kama vile Bustani ya Dunia ya Barafu na Theluji ya Harbin na maeneo ya michezo ya kuteleza kwenye theluji ya Milima Changbai yamekuwa na mchango muhimu katika kuhimiza ongezeko la uchumi.

Mtafiti wa taasisi ya utalii ya China, Han Yuanjun, amesisitiza kwamba uvumbuzi kama huo umedumisha mahitaji makubwa kwa shughuli za utalii kwenye mazingira ya barafu na theluji.

Utafiti wa hivi karibuni wa taasisi hiyo umegundua kuwa asilimia 74.8 ya waliohojiwa wamepanga kushiriki katika shughuli husika za burudani wakati wa majira ya baridi ya 2025-2026, na asilimia 50.5 wanapenda kufanya safari ndefu ya utalii katika majira ya baridi.

Ameeleza kuwa matumizi ya watalii yanabadilika kutoka "gharama halisi" za kawaida kama vile usafiri na malazi hadi "gharama laini" zaidi kama vile burudani, uzoefu wa kitamaduni na teknolojia, ikionyesha mabadiliko katika vyote ubora na muundo wa utalii wa majira ya baridi nchini China.

Ripoti hiyo pia imeeleza kuwa, mahitaji ya burudani ya barafu na theluji ndani ya majengo yanaongezeka, ambapo maeneo ya kusini mwa China yakiwekeza yuan bilioni 30 katika sekta hiyo mwaka 2025, ikichukua asilimia 30 ya jumla. Maeneo hayo husika ya ndani yamekuwa eneo muhimu la uwekezaji, na kuongeza mahitaji ya utalii wa mwaka mzima.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha