Treni ya mizigo ya usafirishaji kwenye reli na baharini iliyopakia magari yanayotumia nishati mpya yaondoka Chongqing, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 08, 2026
Treni ya mizigo ya usafirishaji kwenye reli na baharini iliyopakia magari yanayotumia nishati mpya yaondoka Chongqing, China
Treni ya mizigo iliyopakia magari yanayotumia nishati mpya yaliyoundwa Chongqing ikisubiri kuondoka katika Stesheni ya Reli ya Yuzui ya Bandari ya Guoyuan huko Chongqing, kusini magharibi mwa China, Januari 7, 2026. (Xinhua/Tang Yi)

Treni ya mizigo iliyopakia magari yanayotumia nishati mpya yaliyoundwa Chongqing imeondoka jana Jumatano, katika Stesheni ya Reli ya Yuzui ya Bandari ya Guoyuan huko Chongqing, kusini magharibi mwa China. Treni hiyo inatazamiwa kufika kwenye Bandari ya Nansha la Mji wa Guangzhou kusini mwa China baada ya saa 48 na kisha kuhamishiwa kwenye meli inayoelekea Mashariki ya Kati.

Mji wa Chongqing ambao ni kituo kikuu cha viwanda vya kuunda magari, umekuwa ukiendesha kwa utulivu treni za mizigo za usafirishaji kwenye njia za reli na baharini zinazoelekea mashariki na kusini mwa China kupitia Mji wa Ningbo katika Mkoa wa Zhejiang, mashariki mwa China na Mji wa Qinzhou katika Mkoa Unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi, kusini mwa China.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha