Lugha Nyingine
Meli ya kitalii “Lixiang” yenye uzito wa zaidi ya tani 100,000 yafanyiwa matengenezo mjini Qingdao
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 09, 2026
Kwa sasa, meli kubwa ya kitalii “Lixiang” inafanyiwa matengenezo kwa utaratibu katika kiwanda cha Kampuni ya Uundaji Meli ya Beihai ya Qingdao chini ya Shirika la Uundaji Meli la China. “Lixiang” ni meli ya kitalii yenye jumla ya uzito wa tani 103,000 iliyoundwa na kiwanda cha kuunda meli cha Fincantieri cha Italia, na iliwasili katika kiwanda hicho Desemba 24, 2025 kwa ajili ya matengenezo ya kawaida.
Huu ni mradi wa pili wa matengenezo ya meli kubwa ya kitalii kufanywa na kampuni hiyo, kufuatia mradi wa meli ya kitalii “Mengxiang”, ikiashiria kiwango kipya cha uwezo wa huduma kwa sekta ya meli za kitalii mjini Qingdao.
(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




