Lugha Nyingine
Kiasi cha mizigo kinachopita kwenye Bandari ya Ningbo-Zhoushan ya China chazidi tani bilioni 1.4 katika mwaka 2025
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 09, 2026
![]() |
| Picha hii iliyopigwa Januari 8, 2026 ikionyesha meli ya mizigo ikitia nanga katika eneo la Meishan la Bandari ya Ningbo-Zhoushan, Mkoa wa Zhejiang, mashariki mwa China. (Xinhua/Huang Zongzhi) |
Bandari ya Ningbo-Zhoushan ya China ambayo ni kituo muhimu cha Njia ya Hariri ya Baharini ya Karne ya 21, imeendelea kupanua wigo wa mtandao wake wa usafirishaji duniani. Hadi mwishoni mwa mwaka 2025, bandari hiyo ilikuwa na njia zaidi ya 300 za usafirishaji wa makontena kwa meli, zikiunganisha bandari zaidi ya 700 katika nchi na maeneo zaidi ya 200.
Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa hivi karibuni, Bandari ya Ningbo-Zhoushan ilishuhudia kiasi chake cha mizigo kinachopitishwa kikizidi tani bilioni 1.4 mwaka 2025, ikishikilia nafasi ya kwanza duniani kwa miaka 17 mfululizo.
(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




