Alikimbia kwa kasi kumwokoa mtoto swala wa Tibet aliyeanguka majini (9)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 14, 2026
Alikimbia kwa kasi kumwokoa mtoto swala wa Tibet aliyeanguka majini
Kundi la swala wa Kitibet na watoto wao wanavuka Mto Senlong Zangbo, Mkoa unaojiendesha wa Xizang, Julai 15, 2025. (Xinhua)

Mwezi Julai mwaka 2025, nilifika Kituo cha Usimamizi cha Cuoromu cha Idara ya Usimamizi ya Eneo la Nagqu, katika Hifadhi ya Kitaifa ya Mazingira ya Asili ya Qiangtang, mkoani Xizang.

Tukifunga safari kutoka kituo hicho na kuendesha gari kwa kilomita 50 kwenye mbuga usio na barabara, wakati gari liliposimama tu, nilimwona dereva Tsewang akishuka chini kutoka gari mara akakimbia kwa kasi sana na kufika kando ya mto, akaruka majini mara moja na kumwokoa mtoto swala wa Kitibet aliyekubwa na mawimbi ya kasi mtoni.

Hifadhi ya Kitaifa ya Mazingira ya Asili ya Qiangtang iko kwenye eneo lenye wastani wa mwinuko wa zaidi ya mita 4,500 kutoka usawa wa bahari, hali ya hewa ni mbaya sana, na wastani wa halijoto ya mwaka ilifika nyuzi joto chini ya sifuri. Hata hivyo, eneo hili ni makazi ya wanyamapori wengi wa aina 10 za ulinzi wa ngazi ya kwanza ya kitaifa, na aina 21 za ulinzi wa ngazi ya pili ya kitaifa.

Kuanzia mwaka 2015, Mkoa unaojiendesha wa Xizang umeanzisha vituo 73 vya ulinzi wa wanyamapori katika eneo la Qiangtang, na hivi sasa kuna walinzi wataalamu wa wanyamapori zaidi ya 780.

Kila ufikapo mwezi wa Julai, watoto swala wa Kitibet wanaozaliwa katika eneo la ndani la Qiangtang wanafuatana na mama zao kuhama hadi makazi yao ya zamani. Swala wengi wa Xizang wanakusanyika katika kando ya magharibi ya Mto Senlong Zangbo, na kuvuka mto mfululizo, ambapo hali yao ya uhamiaji inavutia sana na inaendelea kuonekana kwa muda wa wiki moja hivi.

Kwa maelezo ya Awang Lodro, mkuu wa Kituo cha Usimamizi cha Cuoromu, katika miaka mitatu ya hivi karibuni iliyopita, idadi ya swala wa Kitibet wanaovuka mto kutoka hapo imezidi 150,000 kwa mwaka.

Sehemu nyembamba zaidi katika Mto Senlong Zangbo ina upana wa mita moja tu, lakini mawimbi ya maji ni ya kasi sana. Kabla ya watoto swala kuvuka mto, mama swala wanahitaji kufanya majaribio ya kuvuka njia hii kwa mara nyingi, halafu kuwaongoza watoto kuruka au kutembea majini katika sehemu salama. Kila mwaka wapo maelfu ya watoto swala wa Kitibet wanashindwa kuvuka kwa sababu ya mawimbi ya kasi ya maji, na kusababisha kutengana na kundi lake hata kupoteza maisha majini. Wafanyakazi wa Kituo cha Usimamizi cha Cuoromu wameokoa watoto wa swala katika sehemu ya mtiririko wa chini wa maji ya mto kwa miaka mingi. Wale wanaoshindwa kurudi kundi lao wanahifadhiwa katika kituo hicho hadi wanapoweza kula nyasi wenyewe.

Kutokana na hatua za ulinzi wenye nguvu, idadi ya swala wa Kitibet imeendelea kuongezeka katika miaka ya hivi karibuni. Ripoti ya Hali ya Mazingira ya Asili ya Mkoa unaojiendesha wa Xizang ya Mwaka 2023 iliyotolewa na Ofisi Kuu ya Mazingira Ikolojia ya Mkoa unaojiendesha wa Xizang mwaka 2024, inaonyesha kwamba idadi ya swala wa Kitibet katika mkoa wa Xizang imeongezeka hadi zaidi ya 300,000. Ni kwa sababu ya juhudi za hao watu wa kawaida za kulinda wanyama bila ya kujali chochote katika uwanda wa juu wenye theluji, ndipo mafanikio haya yanapoweza kupatikana.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha