Lugha Nyingine
Waziri Mkuu wa Canada awasili Beijing kwa ziara ya kiserikali (3)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 15, 2026
![]() |
| Waziri Mkuu wa Canada Mark Carney akiwasili Beijing, mji mkuu wa China, Januari 14, 2026. (Xinhua/Cai Yang) |
BEIJING - Waziri Mkuu wa Canada Mark Carney amewasili Beijing jana Jumatano kwa ziara ya kiserikali nchini China itakayoendelea hadi siku ya Jumamosi wiki hii. Hii ni mara ya kwanza kwa waziri mkuu wa Canada kufanya ziara nchini China katika miaka minane iliyopita.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China alipojulisha ziara hiyo ya Carney alisema, China inatarajia kutumia ziara yake hiyo kama fursa ya kuzidisha mazungumzo na mawasiliano, kuongeza hali ya kuaminiana kisiasa, kupanua ushirikiano wenye matokeo halisi, kushughulikia tofauti kwa mwafaka, kujadili masuala yanayofuatiliwa na kila mmoja na kuimarisha mwelekeo wa kuboresha uhusiano kati ya China na Canada ili kuleta manufaa zaidi kwa watu wa nchi hizo mbili.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




