Lugha Nyingine
Eneo wazi lisilotumika labadilishwa kuwa bustani maalum ya paka vipenzi wa binadamu katika Mji wa Chongqing
![]() |
| Watalii wakipiga picha kwa paka kwenye bustani maalum ya paka vipenzi wa binadamu katika Eneo la Nan'an, Chongqing, kusini magharibi mwa China, Januari 5, 2026. (Picha na Guo Xu/Xinhua) |
Tangu mwaka 2025, eneo wazi lisilotumika kando ya Mto Yangtze katika Eneo la Nan'an la Mji wa Chongqing kusini magharibi mwa China imebadilishwa kuwa bustani maalum ya paka vipenzi wa binadamu. Ikiwa na ukubwa wa mita za mraba 30,000, bustani hiyo hutumika kama hifadhi salama kwa paka waliotelekezwa au kujeruhiwa.
Baada ya kupata matibabu na chanjo, paka wenye afya njema huzurura kwa uhuru katika maeneo ya wazi ili kuchangamana na watalii, huku wale wenye ulemavu wakipata huduma kwenye eneo lililotengwa kwa ajili ya kuwahudumia.
Ili kuhakikisha usalama, bustani hiyo ina wafanyakazi wataaluma zaidi ya 40, wakiwemo madaktari wa mifugo na watunzaji, ambao hufanya upimaji wa afya kila siku na kuongoza watalii juu ya mchangamano unaofaa.
Hadi sasa hifadhi hiyo salama imeokoa paka zaidi ya 600 waliotelekezwa au kupotea. Tangu kufunguliwa kwa umma mapema Januari, paka zaidi ya 50 wamepata makazi yao mapya.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




