Lugha Nyingine
Sehemu ya kaskazini ya awamu ya kwanza ya Reli ya Usafiri wa Umma ya Njia No. Z4 ya Tianjin, China yaanza kutoa huduma (2)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 19, 2026
![]() |
| Dreva wa Reli ya Usafiri wa Umma ya Njia No. Z4, akijiandaa kabla ya kuanza kutoa huduma mjini Tianjin, Januari 18, 2026. (Xinhua/Zhao Zishuo) |
Sehemu ya kaskazini ya awamu ya kwanza ya Reli ya Usafiri wa Umma ya Njia No. Z4 Mji wa Tianjin, Kaskazini mwa China imeanza kutoa huduma rasmi jana Jumapili.
Sehemu hiyo mpya iliyofunguliwa ina urefu wa kilomita 23.7 ikiwa na stesheni 10. Baada ya kukamilika, njia yote ya Awamu ya kwanza ya reli hiyo itakuwa na urefu wa jumla wa kilomita 43.7 na stesheni 24.
Njia hiyo ya reli ni uti wa mgongo unaounganisha sehemu za kaskazini, kusini na katikati za Eneo Jipya la Binhai, inatarajiwa kubeba jukumu muhimu katika kuboresha mfumo wa usafiri wa reli wa eneo husika na kuhimiza mafungamano.
(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




