Lugha Nyingine
Mkoa wa Hainan wa China washuhudia abiria wanaoingia na kutoka zaidi ya 310,000 tangu uendeshaji maalum wa forodha kuanza (2)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 19, 2026
![]() |
| Abiria wa kigeni wakisubiri taratibu za ukaguzi wa mpakani kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Sanya Phoenix mjini Sanya, Mkoa wa Hainan, kusini mwa China, Januari 15, 2026. (Xinhua) |
Mwezi mmoja baada ya uendeshaji maalum wa forodha kisiwani kote kuanza, Bandari ya Biashara Huria ya Hainan (FTP) katika Mkoa wa Hainan, kusini mwa China imepata mafanikio ya awali katika kuongeza urahisi kwa abiria
Kwa mujibu wa takwimu, kisiwa hicho kimeshuhudia wageni wanaoingia na kutoka zaidi ya 310,000 katika mwezi wa kwanza tangu uendeshaji huo maalum wa forodha uanze.
Takwimu hizo zinaonesha kuwa, raia wa kigeni wamechukua asilimia 59 ya watu hao wote waliovuka mpaka kwa kuwa na idadi ya wageni walioingia na kutoka 186,000. Wakati huo huo, sera za kuingia kwa msamaha wa visa zimekaribisha wasafiri wa kigeni takribani 87,000 kwenda Hainan, ambayo ni sawa na asilimia 93 ya wageni wote waliofika katika mkoa huo.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




