Lugha Nyingine
Maelfu ya samaki wakirukaruka, watu wapata uzoefu wa uvuvi wa majira ya baridi katika ziwa la mpaka wa China na Russia (3)
![]() |
| Mvuvi anaonyesha samaki mkubwa aliyekamatwa wakati wa Tamasha la Uvuvi wa Majira ya Baridi la Ziwa Xingkai la mwaka 2026, Januari 17. (Xinhua/Zhang Tao) |
Tamasha la Uvuvi wa Majira ya Baridi la Ziwa Xingkai la mwaka 2026 lilifunguliwa Januari 17 kando ya Ziwa Xingkai, ambalo liko mpakani kati ya China na Russia. Watu walishuhudia kwa pamoja tukio la kuvutia ambapo wavu mkubwa wenye urefu wa karibu kilomita moja kutoka barafu na kuibuka juu ya uso wa ziwa, huku maelfu ya samaki walirukaruka kwa shamrashamra. Tukio hilo liliwawezesha watu kujionea urithi wa utamaduni wa uvuvi na uwindaji wa Wasushen unaodumu kwa zaidi ya milenia, na kuhisi mvuto wa kipekee wa utamaduni wa barafu na theluji wa maeneo ya mpakani ya kaskazini.
Tamasha la mwaka huu linafanyika chini ya dhana ya maendeleo jumuishi ya “utamaduni, michezo na utalii”, kwa kuunda kwa makini mfumo wa uzoefu wa kushirikisha wageni katika mnyororo mzima wa shughuli, na kubadilisha “rasilimali za baridi” kuwa “sekta zenye mvuto na uhai wa kiuchumi”.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




