Lugha Nyingine
IMF yapandisha makadirio ya ukuaji wa uchumi duniani katika mwaka 2026
(CRI Online) Januari 20, 2026
Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) limetoa marekebisho ya Ripoti ya Makadirio ya Uchumi Duniani jana Jumatatu, likipandisha kidogo makadirio ya ukuaji wa uchumi wa dunia katika mwaka 2026.
Pia limeeleza kuwa, mivutano ya kibiashara na kuongezeka kwa migogoro ya siasa za kijiografia vitaweza kuleta shinikizo kubwa zaidi kwa shughuli za uchumi duniani.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, mwaka 2026 uchumi wa dunia utaongezeka kwa asilimia 3.3, ikiwa ni ongezeko la asilimia 0.2 kuliko makadirio yaliyotolewa mwezi Oktoba mwaka jana, na unatarajiwa kuongezeka kwa asilimia 3.2 katika mwaka 2027, sawa na makadirio ya mwezi Oktoba mwaka jana.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



