Spika wa Bunge la Umma la China afanya mazungumzo na Spika wa Bunge la Taifa la Pakistan

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 20, 2026

Zhao Leji, Spika wa Bunge la Umma la China akifanya mazungumzo na Sardar Ayaz Sadiq, Spika wa Bunge la Taifa la Pakistan katika Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, mji mkuu wa China, Januari 19. 2026. (Xinhua/Liu Weibing)

Zhao Leji, Spika wa Bunge la Umma la China akifanya mazungumzo na Sardar Ayaz Sadiq, Spika wa Bunge la Taifa la Pakistan katika Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, mji mkuu wa China, Januari 19. 2026. (Xinhua/Liu Weibing)

BEIJING - Zhao Leji, Spika wa Bunge la Umma la China, amefanya mazungumzo na Sardar Ayaz Sadiq, Spika wa Bunge la Taifa la Pakistan, mjini Beijing, mji mkuu wa China jana Jumatatu.

Akieleza kuwa mwaka huu ni wa maadhimisho ya miaka 75 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili, Zhao amesema China inapenda kushirikiana na Pakistan kutekeleza maafikiano muhimu yaliyofikiwa na viongozi wa nchi hizo mbili, kuharakisha ujenzi wa jumuiya ya China na Pakistan yenye mustakabali wa pamoja iliyo karibu zaidi katika zama mpya, na kuleta manufaa makubwa zaidi kwa watu wa nchi hizo mbili.

Zhao amesema kwamba China ina nia ya kuimarisha kulinganisha Mpango wake wa 15 wa Miaka Mitano na Mpango wa Taifa wa Mageuzi ya Kiuchumi wa Pakistan (URAAN Pakistan) kwa kipindi cha 2024-2029.

Zhao ameongeza kwamba China inapenda kusukuma mbele toleo 2.0 la ujenzi wa Ukanda wa Kiuchumi wa China na Pakistan (CPEC), na kuleta mafanikio zaidi katika maeneo muhimu kama vile viwanda, kilimo, madini, usafirishaji na ustawi wa maisha ya watu. Pia amesema kwamba China inaunga mkono juhudi thabiti za Pakistan za kupambana na ugaidi.

"Bunge la Umma la China lina nia ya kuimarisha ubadilishanaji wa uzoefu na Bunge la Pakistan juu ya utawala, utungaji wa sheria, usimamizi na maeneo mengine husika, kwa kuzingatia masuala kama vile ustawishaji wa vijiji na maendeleo ya kijani," Zhao amesema.

Kwa upande wake Sadiq amesema kwamba Pakistan inaunga mkono bila kuyumbayumba msimamo wa China kuhusu maslahi yake ya kimsingi na masuala makuu yanayofuatiliwa, ikiwemo masuala yanayohusiana na Taiwan, Xinjiang na Xizang.

Ameeleza kuwa Pakistan inatarajia kuimarisha ushirikiano na China katika nyanja kama vile uchumi, biashara, uwekezaji, maendeleo ya miundombinu, mawasiliano ya watu kwa watu na mafunzo ya wafanyakazi.

"Bunge la Taifa la Pakistan lina nia ya kuimarisha mawasiliano na ushirikiano wake na Bunge la Umma la China," ameongeza.

Zhao Leji, Spika wa Bunge la Umma la China akifanya mazungumzo na Sardar Ayaz Sadiq, Spika wa Bunge la Taifa la Pakistan kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, mji mkuu wa China, Januari 19. 2026. (Xinhua/Liu Weibing)

Zhao Leji, Spika wa Bunge la Umma la China akifanya mazungumzo na Sardar Ayaz Sadiq, Spika wa Bunge la Taifa la Pakistan kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, mji mkuu wa China, Januari 19. 2026. (Xinhua/Liu Weibing)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha