Lugha Nyingine
Idadi ya watu waliofariki yaongezeka kuwa 13 kwenye ajali ya basi la shule la kusafirisha wanafunzi nchini Afrika Kusini

Picha hii iliyopigwa Januari 19, 2026 ikionyesha hali baada ya ajali kugongana kati ya basi dogo la shule na lori, Vanderbijlpark, kusini mwa Johannesburg, Afrika Kusini. (Xinhua)
JOHANNESBURG – Serikali ya Mtaa katika Jimbo la Gauteng, Afrika Kusini imesema kuwa idadi ya watu waliofariki imeongezwa kuwa 13 kwenye ajali ya kugongana kati ya basi dogo la shule la kusafirisha wanafunzi na lori jana Jumatatu asubuhi huko Vanderbijlpark, kusini mwa Johannesburg.
Ripoti za awali zimesema, wanafunzi 11 walitangazwa kufariki kwenye eneo la tukio, na wengine watano waliojeruhiwa vibaya wanatibiwa hospitalini.
Habari za baadaye zimesema kuwa, idadi ya vifo iliongezeka, ambapo mwili wa mwanafunzi mmoja kupatikana ukiwa umekwama chini ya gari lililopinduka, na mtoto mwingine amefariki hospitalini kutokana na kujeruhiwa vibaya.
Na wanafunzi wengine wanne waliojeruhiwa vibaya wanaendelea kulazwa hospitalini, hivi sasa uchunguzi wa sababu za ajali hiyo unaendelea kufanywa.
Akirejelea taarifa kutoka timu ya uchunguzi, Mkuu wa Jimbo la Gauteng Panyaza Lesufi amesema kwamba basi dogo la shule lilikuwa likijaribu kupita magari kadhaa na hivyo kukutana karibu na lori.
"Dereva wa lori alijaribu kuepuka kugongana, lakini alikuwa amechelewa, " ameongeza.
Akiielezea ajali hiyo kuwa "isiyovumilika," Lesufi amehimiza udhibiti mkali kwa shughuli zinazoongezwa siku hadi siku za usafirishaji wa wanafunzi wa shule za binafsi.
Msemaji wa polisi wa jimbo hilo la Gauteng, Mavela Masondo, amesema kwamba basi hilo dogo la shule lilikuwa limebeba wanafunzi wengi zaidi ya idadi inayoruhusiwa kisheria.
"Tukihesabu idadi kwa sasa, inatuambia kwamba Toyota Quantum ilikuwa imebeba wanafunzi kupita kiasi. Kwa sababu wanafunzi tunaowazungumzia ni 17," Masondo amesema, akiongeza kuwa basi hilo dogo limeidhinishwa kubeba abiria 14.
Polisi wamesema madereva wote wawili wamenusurika kwenye ajali hiyo.
Amesema, baada ya kufanyiwa matibabu, dereva wa teksi ya basi hilo dogo atahojiwa rasmi kwa uchunguzi wa mauaji bila kukusudia.
Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, ameelezea huzuni yake kwa vifo vya watu vilivyosababishwa na ajali hiyo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



