Lugha Nyingine
Watoto na wanawake milioni 4.2 nchini Sudan wakabiliwa na utapiamlo mkali mwaka 2026
(CRI Online) Januari 20, 2026
Kundi la Lishe Duniani limeonya katika ripoti yake jana Jumatatu kuwa watoto karibu milioni 4.2 na wanawake wajawazito au wanaonyonyesha, nchini Sudan wanakadiriwa kusumbuliwa na utapiamlo mkali mwaka 2026 huku kukiwa na kuendelea kwa mapigano na kudororoa kwa huduma za msingi.
Ripoti hiyo ya kundi hilo, iliyotolewa kwa uratibu wa Umoja wa Mataifa, inakadiria kuwa watu karibu milioni 8.4 watahitaji msaada wa lishe mwaka huu, wakiwemo watoto milioni 5 walio na umri wa chini ya miaka mitano na wanawake wajawazito au wanaonyonyesha milioni 3.4.
Wakati huohuo, watoto karibu 824,000 walio na umri wa chini ya miaka mitano wanakadiriwa kuteseka na utapiamlo mkali, na kuongeza hatari ya vifo kama hatua za dharura hazitachukuliwa.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



