Lugha Nyingine
Rais aliye madarakani sasa wa Jamhuri ya Afrika ya Kati ashinda katika uchaguzi wa urais
(CRI Online) Januari 20, 2026

Rais aliye madarakani sasa Faustin-Archange Touadera akisalimia watu baada ya tangazo la matokeo ya mwisho ya uchaguzi wa rais huko Bangui, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Januari 19, 2026. (Xinhua)
Baraza la Kikatiba la Jamhuri ya Afrika ya Kati limetangaza matokeo rasmi ya mwisho ya uchaguzi wa urais uliofanyika Desemba 28, 2025, na kumtangaza rais aliye madarakani sasa wa nchi hiyo Faustin-Archange Touadera kuwa mshindi.
Baraza hilo limetangaza jana Jumatatu katika hafla iliyofanyika Bangui, mji mkuu wa nchi hiyo, kwamba, Rais Touadera, aliyepata asilimia 77.90 ya kura, atatumikia kipindi cha miaka saba.
Mamlaka ya Uchaguzi nchini humo imesema, wapiga kura milioni 2.3 walijiandikisha kushiriki uchaguzi huo uliofanyika kwa amani.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



