Lugha Nyingine
Mapato yanayotokana na utalii nchini Tanzania yafikia rekodi ya dola za kimarekani bilioni 4.2
Sekta ya utalii nchini Tanzania imeingiza dola za kimarekani bilioni 4.2 katika mwaka ulioishia Oktoba, 2025, ikiwa ni kiasi cha juu katika historia ya nchi hiyo.
Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Benki Kuu ya Tanzania, ongezeko hilo limetokana na idadi kubwa ya watalii kutoka nchi za nje.
Takwimu rasmi zinaonyesha kuwa, Tanzania imepokea watalii karibu 173,000 wa kigeni kati ya Januari na Novemba, 2025, ikiwa ni idadi kubwa ikilinganishwa na mwaka 2024, na kufanya jumla ya watalii walioingia nchini humo kufikia milioni 2.09, ongezeko la asilimia 9 ikilinganishwa na mwaka 2024.
Akifungua mkutano wa wadau wa sekta ya wanyamapori jijini Dodoma Jumamosi iliyopita, Waziri wa Maliasili na Utalii wa Tanzania, Ashatu Kijaji ameielezea sekta hiyo kuwa ni tulivu na yenye uhai, akirejelea tuzo ambazo sekta hiyo imeshinda kimataifa ambazo zinaakisi ushirikiano imara wa sekta binafsi na umma, na mikakati imara ya masoko na uwekezaji mkubwa katika miundombinu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



