Ubalozi wa China nchini Sudan Kusini watoa msaada wa mashine za kilimo kuongeza usalama wa chakula

(CRI Online) Januari 21, 2026

Ubalozi wa China nchini Sudan Kusini umetoa msaada wa zaidi ya vifaa 20 vya mashine za kilimo ili kuongeza uzalishaji wa chakula katika mkoa wa Ikweta Magharibi nchini humo.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi msaada huo hapo jana, msaidizi wa katibu mkuu wa Wizara ya Ujenzi wa Amani Pia Philip Michael amesema, vifaa hivyo vitaboresha usalama wa chakula na kusaidia juhudi za ujenzi wa amani katika mkoa huo ambao umeshuhudia mapigano ya kikabila tangu mwaka 2021. Amesema mashine hizo zitasaidia mageuzi ya mkoa huo kutoka kilimo cha kujikimu hadi kilimo cha kisasa cha kitaalamu kinacholenga soko.

Naye Balozi wa China nchini Sudan Kusini Ma Qiang amesema, vifaa hivyo vilivyotolewa na kampuni ya Kundi la Zhaotai ni pamoja na matrekta, na mashine za kulima na kupanda, na vinaonyesha uwajibikaji na ahadi ya kampuni za China, na juhudi pana za China kuunga mkono ustawi wa Sudan Kusini na kujenga jamii ya binadamu yenye hatma ya pamoja.

(Wahariri wa tovuti:Zhao Jian)

Picha