Bidhaa zinazotumia nishati ya jua zilizotengenezwa na China zasaidia mageuzi ya kijani barani Afrika

(CRI Online) Januari 21, 2026

Matumizi ya nishati ya kijani barani Afrika yameongezeka kwa kasi kutokana na upatikanaji wa suluhisho la bidhaa za ubora wa juu na gharama nafuu za umeme wa jua zinazotengenezwa nchini China.

Meneja wa mradi katika Kituo cha Uwezo wa Nishati, Mazingira na Uchumi Endelevu katika Kampuni ya Huduma ya AHK East Africa, Georg Pflomm amesema, bidhaa zinazotumia nishati ya jua zinazotengenezwa nchini China zimeboresha upatikanaji wa nishati na usalama katika bara la Afrika linalotaka kuendeleza utoaji mdogo wa hewa ya kaboni.

Amesema China imedumu kuwa na nafasi muhimu katika mnyororo wa thamani wa nishati ya jua duniani, ikinufaisha nchi za Afrika katika haja yao ya kuweka nishati ya kijani katika mikongo yao ya kitaifa.

(Wahariri wa tovuti:Zhao Jian)

Picha