Lugha Nyingine
Rais wa China ampongeza Faustin Archange Touadera kwa kuchaguliwa tena kuwa rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati
Rais wa China Xi Jinping Jumanne ametuma salamu za pongezi kwa Faustin Archange Touadera kwa kuchaguliwa tena kuwa rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Katika salamu hizo, rais Xi ameeleza kuwa, China na Jamhuri ya Afrika ya Kati zimeendelea kuimarisha hali ya kuaminiana kisiasa. Pande hizo mbili zimeungana mkono kithabiti maslahi na masuala makuu ya kila upande, kuhimiza kwa hatua madhubuti ushirikiano katika sekta mbalimbali.
Rais Xi amesisitiza kuwa anathamini sana maendeleo ya uhusiano kati ya China na Jamhuri ya Afrika ya Kati, na yupo tayari kushirikiana na rais Touadera kutekeleza kikamilifu matokeo yaliyopatikana katika mkutano wa viongozi wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika, kuendeleza uhusiano wa kimkakati kati ya nchi hizo mbili katika kiwango kipya, ili kunufaisha zaidi watu wa nchi hizo mbili.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



