Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping asisitiza umuhimu wa kupata mwanzo mzuri wa mpango mpya wa miaka mitano

Rais wa China Xi Jinping, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akihutubia ufunguzi wa semina kwenye Chuo cha Chama cha Kamati Kuu ya CPC (Chuo cha Taifa cha Utawala) kwa maafisa wakuu katika ngazi za mikoa na wizara, Januari 20, 2026. (Xinhua/Xie Huanchi)
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping jana Jumanne wakati akifungua semina kwenye Chuo cha Chama cha Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (Chuo cha Taifa cha Utawala) kwa maafisa wakuu katika ngazi za mikoa na wizara, ametoa wito wa kuchukuliwa juhudi thabiti ili kuhakikisha mwanzo mzuri wa Mpango wa 15 wa Miaka Mitano (2026-2030).
Rais Xi ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) amesema kuwa uundaji na utekelezaji wa mipango ya miaka mitano ni uzoefu muhimu wa Chama katika kutawala nchi na kusimamia masuala ya serikali, vilevile ni nguvu kubwa bora ya kisiasa ya mfumo wa ujamaa wenye umaalum wa China, jambo linalosaidia kudumisha mwendelezo wa sera.
Amesema kuwa, ni muhimu kujenga uelewa wa jumla, wa kina na sahihi kuhusu mipangilio ya kimkakati ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika kipindi cha Mpango wa 15 wa Miaka Mitano, kama ilivyowekwa kwenye mkutano wa nne wa wajumbe wote wa Kamati Kuu ya 20 ya CPC.
Amesisitiza kwamba China kwa sasa iko katika hatua ambayo fursa na hatari za kimkakati zinaambatana, huku hali ya kutokuwa na uhakika na mambo yasiyotabirika ikiongezeka. Ameongeza kuwa kujenga mfumo wa kisasa wa viwanda na kufikia uboreshaji wa jumla wa muundo wa viwanda ni majukumu muhimu ya kimkakati katika kipindi cha Mpango wa 15 wa Miaka Mitano.
Rais Xi amesisitiza umuhimu wa kudumisha uwiano unaofaa wa sekta ya uzalishaji katika uchumi, pamoja na kuendeleza kwa nguvu viwanda vya hali ya juu. Pia amesisitiza umuhimu wa kujenga miundombinu ya kisasa.
"China iko katika nafasi nzuri ya kuharakisha uundaji wake wa muundo mpya wa maendeleo," amesema, akisisitiza kuwa uchumi wa ndani unapaswa kuwa nguzo kuu, na kwamba uwekezaji katika mali halisi unapaswa kuunganishwa kwa karibu na uwekezaji katika mtaji wa rasilimali watu.
Rais Xi amesema kwamba kuboresha maisha ya watu kunapaswa kupewa kipaumbele cha juu ili kuhimiza maendeleo ya kijamii. Ameongeza kuwa, sambamba na kuendeleza ukuaji wa uchumi, juhudi thabiti zinapaswa kufanywa ili kuinua ubora wa maisha ya watu.

Rais wa China Xi Jinping, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akihutubia ufunguzi wa semina kwenye Chuo cha Chama cha Kamati Kuu ya CPC (Chuo cha Taifa cha Utawala) kwa maafisa wakuu katika ngazi za mikoa na wizara, Januari 20, 2026. (Xinhua/Li Xiang)

Rais wa China Xi Jinping, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akihutubia ufunguzi wa semina kwenye Chuo cha Chama cha Kamati Kuu ya CPC (Chuo cha Taifa cha Utawala) kwa maafisa wakuu katika ngazi za mikoa na wizara, Januari 20, 2026. (Xinhua/Li Xiang)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



