Waziri Mkuu wa Greenland asema picha aliyotoa Trump inayoashiria udhibiti wa Marekani juu ya Greenland ni ya kutoheshimu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 21, 2026

Waziri Mkuu wa Greenland Jens-Frederik Nielsen (kushoto, kwenye theluji) akionekana kwenye maandamano ya kupinga maneno na vitendo vya Marekani vinavyoashiria udhibiti juu ya Greenland huko Nuuk, mji mkuu wa Greenland, eneo linalojitawala la Denmark, Januari 17, 2026. (Picha na Anders Kongshaug/Xinhua)

OSLO - Waziri Mkuu wa Greenland Jens-Frederik Nielsen amesema picha aliyotoa Rais wa Marekani Donald Trump iliyoashiria udhibiti wa Marekani juu ya Greenland ni ya kutoheshimu Greenland.

"Bila shaka, tunafuatilia kile kinachoendelea kwenye mitandao ya kijamii, picha hii ni ya kutoheshimu," Nielsen amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Nuuk, mji mkuu wa Greenland jana Jumanne.

"Tunataka mazungumzo kupitia njia zinazofaa, ili yasifanyike kwenye vyombo vya habari na kwenye mitandao ya kijamii," ameongeza.

Picha hii iliyopigwa Januari 16, 2026 ikionyesha mlima karibu na Nuuk, mji mkuu wa Greenland, eneo linalojitawala la Denmark. (Picha na Anders Kongshaug/Xinhua)

Picha hii iliyopigwa Januari 16, 2026 ikionyesha mlima karibu na Nuuk, mji mkuu wa Greenland, eneo linalojitawala la Denmark. (Picha na Anders Kongshaug/Xinhua)

Jana Jumanne Trump alitoa picha moja kwenye jukwaa lake la mtandao wa kijamii la Truth Social, picha hii ambayo inamwonesha akichomeka mlingoti wa bendera ya Marekani kwenye ardhi ya Greenland.

Kwenye picha hiyo, Trump anaonekana akiwa ameambatana na Makamu Rais wa Marekani JD Vance na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio, wakiwa karibu na bango linaloandikwa maneno ya "GREENLAND – ARDHI YA MAREKANI ILIYOANZISHWA 2026." (GREENLAND - US TERRITORY EST. 2026.)

Nielsen amesisitiza kwamba Greenland lazima ijiandae kwa uwezekano wa aina yoyote, kwani Trump hajaondoa uwezekano wa kutumia nguvu. 

Watu wakishiriki kwenye maandamano ya kupinga maneno na vitendo vya Marekani vinavyoashiria udhibiti juu ya Greenland huko Nuuk, mji mkuu wa Greenland, eneo linalojitawala la Denmark, Januari 17, 2026. (Picha na Anders Kongshaug/Xinhua)

Amesisitiza tena kwamba Greenland ni mwanachama wa Jumuiya ya NATO, na operesheni yoyote ya kijeshi itakuwa na athari kubwa kwa maeneo ya nje ya Greenland.

"Katika wakati hali ya Arctic inayozidi kuwa wasiwasi, hakika tunahitaji kuwa na uwepo mkubwa wa kijeshi," Nielsen amesema.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha