China inaunga mkono kithabiti mfumo wa pande nyingi na biashara huria: Naibu Waziri Mkuu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 21, 2026

Naibu Waziri Mkuu wa China He Lifeng, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akitoa hotuba kwenye Mkutano wa Mwaka wa Baraza la Uchumi Duniani (WEF) 2026 mjini Davos, Uswisi, Januari 20, 2026. (Xinhua/Peng Ziyang)

DAVOS, Uswisi – Naibu Waziri Mkuu wa China He Lifeng jana Jumanne wakati akitoa hotuba kwenye Mkutano wa Mwaka wa Baraza la Uchumi Duniani (WEF) 2026 mjini Davos, Uswisi, ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuunga mkono kithabiti mfumo wa pande nyingi na biashara huria, na kudumisha dhamira ya ushirikiano wa kunufaishana.

Huku akikumbushia hotuba ya Rais Xi Jinping wa China iliyotolewa katika WEF Januari 2017, He amesema tangu wakati huo China imeweka maneno yake katika vitendo na kushikilia kithabiti mfumo wa pande nyingi na biashara huria.

Ameongeza kuwa "katika miaka ya hivi karibuni, Rais Xi amependekeza mipango minne ya kimataifa kwa mfululizo, akitoa masuluhisho ya China kwa changamoto za pamoja zinazoikabili dunia."

Akizungumza kwenye baraza hilo, naibu waziri mkuu wa China ametoa mapendekezo manne muhimu. Kwanza, amehimiza jumuiya ya kimataifa kuunga mkono kithabiti biashara huria na kuendeleza utandawazi wa kiuchumi wenye manufaa kwa wote na jumuishi.

Pili, amesema kuwa mfumo wa pande nyingi unapaswa kushikiliwa bila kuyumbayumba, na kwamba ni muhimu kuufanya utaratibu wa kiuchumi na biashara wa kimataifa uwe wa haki na wenye mantiki zaidi.

"Tatu, dunia inapaswa pia kuzingatia ushirikiano wa kunufaishana, kujitolea kuongeza manufaa ya ushirikiano, na kwa pamoja kushughulikia changamoto za maendeleo," ameongeza.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa kuheshimiana na mashauriano kwa misingi ya usawa, na kutoa wito kwa nchi zote kutumia ipasavyo mazungumzo ili kudhibiti tofauti na kutatua masuala kwa njia sahihi.

Naibu Waziri Mkuu wa China He Lifeng, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akihudhuria Mkutano wa Mwaka wa Baraza la Uchumi Duniani (WEF) 2026 mjini Davos, Uswisi, Januari 20, 2026. (Xinhua/Peng Ziyang)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha