Lugha Nyingine
China Bara yasisitiza Maafikiano ya 1992 kuwa msingi wa kurejesha mazungumzo kati ya pande mbili za Mlango-Bahari wa Taiwan

Peng Qing'en, msemaji wa Ofisi ya Masuala ya Taiwan ya Baraza la Serikali la China, akionesha ishara kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Beijing, mji mkuu wa China, Januari 21, 2026. (Xinhua/Pan Xu)
BEIJING - Peng Qing'en, msemaji wa Ofisi ya Masuala ya Taiwan ya Baraza la Serikali la China amesema kwamba ni kwa kutambua tu Maafikiano ya 1992, ambayo yanajumuisha kanuni ya kuwepo kwa China moja, ndipo pande mbili za Mlango-Bahari wa Taiwan zinaweza kurejesha mazungumzo na mifumo ya mazungumzo.
"Maafikiano ya 1992 yanafafanua kwa wazi asili ya uhusiano kati ya Pande mbili za Mlango-Bahari wa Taiwan, na hutumika kama msingi wa kisiasa wa maendeleo ya uhusiano huo, vilevile kuwa nguzo ya amani na utulivu katika Mlango-Bahari," amesema Peng jana Jumatano wakati akitoa maoni kuhusu kauli za hivi karibuni za utawala wa Taiwan kuhusu maafikiano hayo.
Peng ameeleza kwamba Maafikiano ya 1992 yalifikiwa kati ya Shirikisho la Uhusiano kati ya pande mbili za Mlango-Bahari wa Taiwan (ARATS) yenye makao yake China Bara na Mfuko wa Mawasiliano ya Pande mbili za Mlango-Bahari (SEF) yenye makao yake Taiwan kwa kukabidhiwa na idhini kutoka utawala wa pande zote mbili za Mlango Bahari.
"Utawala wa Taiwan hauwezi kuwa haujui historia ya mawasiliano kati ya ARATS na SEF, lakini zinapotosha umma kwa makusudi," Peng amesema.
Peng amesema kwamba historia imeonyesha mara kwa mara kwamba Maafikiano ya 1992 yanapotambuliwa na kanuni ya kuwepo kwa China moja kuzingatiwa, uhusiano kati ya pande mbili za Mlango-Bahari wa Taiwan huimarika na kuendelea kukua, na kuleta manufaa halisi kwa wakazi wa Taiwan.
"Kutoka mwaka 2008 hadi mwaka 2016, ARATS na SEF zilisaini mfululizo wa makubaliano kwa msingi wa Maafikiano ya 1992, ambayo yalileta manufaa halisi na yanayoonekana kwa watu wa pande zote mbili, hasa watu wa Taiwan," ameongeza.
Amesema kwamba tangu Mei 2016, hata hivyo, utawala wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (DPP) zimeendelea kushikilia kwa ukaidi msimamo wa kujitenga, zimekataa kutambua Maafikiano ya 1992, zimeharibu kwa upande mmoja msingi wa kisiasa wa mazungumzo kati ya pande mbili za Mlango-Bahari wa Taiwan, na kwa makusudi zimezuia na kuwekea vikwazo mawasiliano na ushirikiano kati ya pande hizo mbili.

Peng Qing'en, msemaji wa Ofisi ya Masuala ya Taiwan ya Baraza la Serikali la China, akionesha ishara kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Beijing, mji mkuu wa China, Januari 21, 2026. (Xinhua/Pan Xu)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



