Lugha Nyingine
Trump asisitiza juhudi za kuipata Greenland kwa biashara, azikosoa zaidi Ulaya na NATO kwenye Jukwaa la Uchumi Duniani la Davos
Rais wa Marekani Donald Trump akihutubia Mkutano wa Mwaka wa Jukwaa la Uchumi Duniani mjini Davos, Uswisi, Januari 21, 2026. (Xinhua/Lian Yi)
DAVOS, Uswisi - Rais wa Marekani Donald Trump ametoa hotuba kwa mahsusi kwenye mkutano wa mwaka wa Jukwaa la Uchumi Duniani huko Davos, Uswisi, ambapo amehimiza tena ajenda ya Marekani ya kuipata Greenland kwa biashara, na amezikosoa vikali Ulaya na Jumuiya ya NATO, hivyo hali mpya ya wasiwasi itaonekana kwenye uhusiano kati ya nchi za pande za Atlantiki.
Trump amesema Ulaya "haielekei kwa mwelekeo sahihi," na anaona baadhi ya sehemu za bara hilo zimebadilika hata kuwa sehemu "zisizoweza kutambulika", akielezea hali hiyo kwa namna inayoonekana ya "hasi sana".
Kwenye hotuba yake hiyo, Trump amekosoa kwa mara nyingine tena sera za uhamiaji za Ulaya, na pia amesisitiza kupinga sera za ajenda ya kijani, akiziita tena "Ulaghai Mpya wa Kijani."
Pia ametetea kupanua uzalishaji wa mafuta ya visukuku na kuharakisha idhini za miradi mipya ya nishati ya nyuklia, akisema hali ya nishati ya Ulaya imefikia kiwango cha "kibalaa"ambayo imeonekana kuwa na bei za juu na utoaji usio wa kutosha.
Kuhusu Greenland, Trump ametoa wito wa kufanya mara moja mazungumzo juu ya Marekani kupata eneo hilo kwa biashara, akilielezea kuwa ni "maslahi ya kimkakati ya usalama wa nchi na kimataifa."
Ameondoa hadharani uwezekano wa kuipata Greenland kwa nguvu ya kijeshi, akisema hana nia ya kutumia "nguvu ya kupita kiasi," huku akisisitiza kwamba Marekani iko katika nafasi ya kipekee ya kulipata eneo hilo.
"Sihitaji kutumia nguvu ya kijeshi. Sitaki kutumia nguvu ya kijeshi, na siwezi kutumia nguvu. Marekani inachoomba tu ni sehemu moja inayoitwa Greenland," amesema.
Trump amekosoa zaidi uchangiaji mzigo wa gharama za NATO, akisema Marekani imekuwa ikitendewa "isivyo usawa sana" na kwa muda mrefu imekuwa ikichangia zaidi kwenye jumuiya hiyo kuliko washirika wake wengine, huku akizihimiza nchi wanachama wa NATO kukubali Marekani kuipata Greenland kwa biashara kutoka Denmark.
"Kwa maoni yangu, tulilipa asilimia 100 ya matumizi ya NATO kwa sababu hawakuwa wakilipa bili zao, na tunachoomba ni kuipata Greenland tu, ikiwa ni pamoja na haki ya umiliki, kwa sababu kufanya ulinzi kunahitaji haki ya umiliki," amesema.
Rais wa Marekani Donald Trump akihutubia Mkutano wa Mwaka wa Jukwaa la Uchumi Duniani mjini Davos, Uswisi, Januari 21, 2026. (Xinhua/Lian Yi)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



