Lugha Nyingine
Iran yatangaza rasmi vifo vya watu 3,117 katika ghasia za hivi karibuni
Kituo cha Televisheni cha Iran, IRIB kikinukuu taarifa kutoka Baraza la Usalama wa Taifa la Iran, kimeripoti jana Jumatano kuwa watu 3,117 walifariki katika ghasia za hivi karibuni nchini humo.
Idadi hiyo ni ya kwanza rasmi ya vifo kutolewa na mamlaka za Iran tangu maandamano yalipoanza nchini humo mwishoni mwa Desemba mwaka jana. Maafisa wa Iran hapo awali walikuwa wamekiri kutokea kwa vifo "vingi" bila kutoa idadi kamili.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, watu 2,427 kati ya hao waliouawa wameelezewa kuwa ni "raia na wafanyakazi wa vikosi vya usalama wasio na hatia."
Katika ripoti nyingine, shirika la habari la Tasnim ambalo linamilikiwa kwa sehemu na Serikali ya Iran limeripoti kuwa majengo zaidi ya 460 ya serikali yalibomolewa au kuchomwa moto wakati wa maandamano hayo, huku benki zaidi ya 700 zikishambuliwa au kuchomwa moto. Limeongeza kuwa misikiti zaidi ya 480 pia ililengwa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



