Rais wa Marekani aachana na mpango wa ushuru wa Februari Mosi

(CRI Online) Januari 22, 2026

Rais wa Marekani Donald Trump amesema, mazungumzo yake na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya Nchi za Magharibi (NATO) Mark Rutte yametoa mfumo wa makubaliano ya baadaye kuhusu Greenland na eneo pana la Aktiki, na kutangaza kuwa hataendelea na ushuru kwa nchi nane za Ulaya uliopangwa kuanza kutekelezwa Februari Mosi.

Katika ujumbe wake kwenye jukwaa lake la mtandao wa kijamii la Truth Social, Rais Trump amesema mfumo huo umepatikana kupitia mazungumzo na Rutte na utakuwa bora kwa Marekani na nchi wanachama wa NATO kwa ujumla.

Amesema kutokana na maelewano hayo, hataendelea kutoza ushuru huo kwa nchi za Ulaya uliopangwa kutekelezwa Februari Mosi.

Kabla ya kuhudhuria Mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani mjini Davos, Rais Trump alitishia ushuru mpya kwa nchi nane za Ulaya ikiwemo Denmark na nchi wanachama wa NATO zikiwemo Uingereza, Ufaransa, na Ujerumani.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha