Watu watano wauawa kwa kupigwa risasi katika Jimbo la Gauteng nchini Afrika Kusini

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 22, 2026

Maofisa wa polisi wakifanya kazi kwenye eneo la tukio la ufyatuaji risasi huko Jeffsville, Atteridgeville, Jimbo la Gauteng, Afrika Kusini, Januari 21, 2026. (Picha na Shiraaz Mohamed/Xinhua)

JOHANNESBURG – Polisi nchini Afrika Kusini wamesema katika taarifa yao kuwa watu watano wamepigwa risasi na kufariki dunia jana Jumatano nje ya duka la mizigo huko Jeffsville, Atteridgeville, katika Jimbo la Gauteng nchini humo.

"Tukio hilo lilitokea majira ya saa 7:15 mchana kwa saa za Afrika Kusini (1115 GMT), na wahudumu wa afya wametangaza waathiriwa wote watano wamefariki dunia kwenye eneo la tukio," imesema taarifa hiyo.

Polisi wameeleza kuwa idadi isiyojulikana ya washukiwa waliwakaribia waathiriwa, wakawafyatulia risasi bila kusema maneno yoyote, kisha wakatokomea. Wamesema kwamba nia ya mauaji hayo bado haijulikani, na kwamba uchunguzi unaendelea kufanyika.

Shirika la Utangazaji la Afrika Kusini, likimnukuu Mkuu wa Ofisi ya Polisi ya Afrika Kusini katika Wilaya ya Tshwane Samuel Thine, limeripoti kwamba watatu kati ya watu hao watano waliofariki dunia wametambuliwa na wanaaminika kuwa ni raia wa kigeni.

Watu wakiwa wamekusanyika kwenye eneo la tukio la ufyatuaji risasi huko Jeffsville, Atteridgeville, Jimbo la Gauteng, Afrika Kusini, Januari 21, 2026. (Picha na Shiraaz Mohamed/Xinhua)

Maofisa wa polisi wakilinda eneo la tukio la ufyatuaji risasi huko Jeffsville, Atteridgeville, Jimbo la Gauteng, Afrika Kusini, Januari 21, 2026. (Picha na Shiraaz Mohamed/Xinhua)

Picha hii iliyopigwa Januari 21, 2026 ikionyesha eneo la tukio la ufyatuaji risasi huko Jeffsville, Atteridgeville, Jimbo la Gauteng, Afrika Kusini. (Picha na Shiraaz Mohamed/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha