Lugha Nyingine
Rais wa Uganda apongeza uhusiano unaoongezeka kati ya Uganda na China
(CRI Online) Januari 22, 2026
Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema, uhusiano kati ya Uganda na China umeendelea kuimarika katika miaka ya hivi karibuni, na kwamba sera ya China ya kutoza ushuru-sifuri wa forodha kwa nchi za Afrika itasaidia kuongeza mauzo ya nje ya bidhaa za Uganda nchini China.
Katika taarifa iliyotolewa jana Jumatano na Ikulu ya Uganda, Rais Museveni amepongeza uamuzi wa serikali ya China wa kuondoa ushuru wa forodha kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka Uganda, akisema hatua hiyo itaunga mkono kwa kiasi kikubwa ukuaji wa biashara na jitihada za kutengeneza utajiri za Uganda.
Akizungumzia uwekezaji wa China nchini Uganda, Rais Museveni amesisitiza kuwa Uganda imekuwa ikiunga mkono maslahi ya China, na itaendelea kufanya hivyo.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



