Lugha Nyingine
IGAD yaipongeza Somalia kwa kuidhinisha mkataba mpya wa kuimarisha amani
Mamlaka ya Kiserikali kwa ajili ya Maendeleo ya Nchi za Afrika Mashariki (IGAD) imekaribisha kuidhinishwa kwa Mkataba mpya wa IGAD kulikofanywa na Bunge la Somalia, ikisema hatua hiyo itaongeza kasi ya ushirikiano wa kikanda.
IGAD imesema katika taarifa yake ya jana Jumatano kuwa uidhinishaji huo wa bunge ni mwanzo wa hatua muhimu kwa ushiriki wa Somalia katika mifumo ya kikanda kwa ajili ya amani, maendeleo na ushirikiano.
Mkataba huo mpya uliofikiwa Juni, 2023, unakuwa mbadala wa makubaliano ya awali ya mwaka 1999 na unalenga kuimarisha mafungamano ya kikanda, kujikita katika amani, usalama, kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, maendeleo ya uchumi, na utawala wa kidijitali.
IGAD imesema, kwa kujiunga na nchi nyingine wanachama ambazo ni Djibouti, Ethiopia, Sudan Kusini na Kenya, katika kuidhinisha mkataba huo mpya wa IGAD, Somalia imethibitisha tena uungaji mkono wake kwa matarajio ya pamoja ya kikanda na kanuni za kuheshimiana, uhusiano, na maendeleo endelevu yanayojikita katika mfumo wa IGAD.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



