Lugha Nyingine
Wawekezaji wa China wavutiwa na uwekezaji katika sekta za miundombinu na kilimo nchini Kenya
Kundi la wawekezaji kutoka China liko nchini Kenya kutafiti fursa za uwekezaji katika sekta za miundombinu na kilimo nchini humo.
Mwanzilishi na mwenyekiti wa kundi la ushawishi wa biashara la China, Fortune Generation, Martin Hang amesema wawekezaji wa China wanachukua nafasi muhimu katika kuboresha miundombinu na katika sekta ya usalama wa chakula nchini Kenya. Amesema wawekezaji wa China wana uwezo wa teknolojia na fedha kujenga barabara za kisasa, bandari, na viwanda vya kuzalisha nishati.
Kaimu meneja wa uwekezaji na mawasiliano ya kibiashara katika Mamlaka ya Maeneo ya Kusindika Bidhaa za Kuuzwa Nje ya Kenya, Moses Kipkebut amesema, Kenya inatafuta kufaidika kutokana na uzoefu wa China katika kuongeza thamani ya bidhaa za kilimo.
Ameongeza kuwa, Kenya imeandaa kanuni rafiki za ushuru katika maeneo ya kusindika bidhaa za kuuzwa nje ili kuwezesha wawekezaji wa kigeni kusaidia kuibadili nchi hiyo kuwa kituo cha kikanda cha kuongeza thamani ya bidhaa za kilimo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



