Uwekezaji wa moja kwa moja wa China kwenda nchi za nje wadumisha ukuaji tulivu katika mwaka 2025

(CRI Online) Januari 23, 2026

Wizara ya Biashara ya China Alhamisi imetangaza kuwa uwekezaji wa moja kwa moja wa China kwenda nchi za nje umezidi dola za kimarekani bilioni 174, ikiwa ni ongezeko la asilimia 7.1 ukiendelea kushika nafasi za mwanzo duniani.

Wizara hiyo imesema, hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2025, China ilikuwa imeanzisha kampuni zaidi ya elfu 5 katika nchi na maeneo 190 duniani, na thamani ya uwekezaji katika nchi za nje imedumisha nafasi tatu za mwanzo katika miaka 9 mfululizo.

Msemaji wa Wizara ya Biashara ya China He Yongqian amesema mwaka 2026 ni mwanzo wa Mpango wa 15 wa Maendeleo wa Miaka Mitano, na Wizara hiyo itatekeleza kwa ufanisi usimamizi wa uwekezaji wa kigeni, kuboresha mfumo wa huduma za jumla za kimataifa, kuhimiza maendeleo yanayofungamanisha biashara na uwekezaji, kuunga mkono kampuni kuendesha shughuli za kimataifa, kuimarisha ushirikiano katika sekta mpya za uchumi wa kidijitali na maendeleo ya kijani, na kuchangia zaidi ukuaji thabiti wa uchumi duniani.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha