Trump aanzisha "Bodi ya Amani" mjini Davos huku akikosolewa kwa kudhoofisha Umoja wa Mataifa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 23, 2026

Rais wa Marekani Donald Trump ameanzisha Bodi ya Amani kwenye hafla ya kutia saini kwenye katiba ya bodi hiyo iliyofanyika wakati wa Jukwaa la Uchumi Duniani (WEF) 2026 mjini Davos, Uswisi, Januari 22, 2026. (Xinhua/Lian Yi)

DAVOS, Uswisi - Rais wa Marekani Donald Trump amezindua rasmi kile kinachoitwa "Bodi ya Amani" katika hafla ya kutia saini kwenye katiba ya bodi hiyo iliyofanyika jana Alhamisi katika wakati wa Jukwaa la Uchumi Duniani (WEF) 2026 mjini Davos, Uswisi.

Hatua hiyo imewafanya waangalizi waone wasiwasi, ambao wanaonya kuwa inaweza kudhoofisha hadhi kuu ya Umoja wa Mataifa na mfumo ulioanzishwa wa pande nyingi wa kulinda amani. Baadhi ya nchi kubwa duniani na washirika wa jadi wa Marekani zimekataa kujiunga na bodi hiyo.

Akizungumza katika hafla hiyo, Trump amesema kwamba bodi hiyo, ambayo ataiongoza, inaweza "kufanya zaidi chochote tunachotaka," huku akidai itafanya kazi "kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa." Hata hivyo, wakosoaji wanaogopa kwamba ina hatari ya kuingiliana au kudhoofisha mfumo uliopo wa pande nyingi unaozingatia Umoja wa Mataifa.

Chini ya mpango wa sasa, Trump atakuwa mwenyekiti wa kwanza wa bodi hiyo, nafasi ambayo anaweza kuishikilia maisha yake yote. Trump amesema nchi wanachama wa kudumu lazima kila moja ichangie dola bilioni 1 za Marekani kufadhili bodi hiyo.

Rais wa Marekani Donald Trump akitoa hotuba kwenye Mkutano wa Mwaka wa Jukwaa la Uchumi Duniani (WEF) 2026 mjini Davos, Uswisi, Januari 22, 2026. (Xinhua/Lian Yi)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha