Denmark yasema Katibu Mkuu wa NATO hana haki ya kufanya mazungumzo juu ya Greenland

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 23, 2026

Waziri Mkuu wa Denmark Mette Frederiksen akihudhuria mkutano maalum wa viongozi wa Umoja wa Ulaya (EU) mjini Brussels, Ubelgiji, Machi 6, 2025. (Xinhua/Peng Ziyang)

Waziri Mkuu wa Denmark Mette Frederiksen akihudhuria mkutano maalum wa viongozi wa Umoja wa Ulaya (EU) mjini Brussels, Ubelgiji, Machi 6, 2025. (Xinhua/Peng Ziyang)

OSLO - Waziri Mkuu wa Denmark Mette Frederiksen amesema kwamba Katibu Mkuu wa Jumuiya ya NATO Mark Rutte hakukabidhiwa na madaraka ya kuiwakilisha Denmark au Greenland kufanya mazungumzo.

Maneno hayo aliyosema jana Alhamisi baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kusema juzi Jumatano kwamba mkutano wake na Rutte umepata maendeleo kuhusu "mfumo wa makubaliano ya siku za baadaye" juu ya Greenland na eneo pana la Arctic.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya NATO Mark Rutte akihudhuria mkutano na waandishi wa habari wakati wa mkutano wa viongozi wa nchi wanachama wa NATO mjini The Hague, Uholanzi, Juni 25, 2025. (Xinhua/Zhao Dingzhe)

Frederiksen ameviambia vyombo vya habari vya Denmark kwamba ingawa Denmark imefanya uratibu na washirika wa pande mbalimbali, akiwemo Rutte, ili kukabiliana pamoja na changamoto zinazoikabili Greenland, na Rutte hajapewa madaraka ya kuiwakilisha Denmark au Greenland kufanya mazungumzo.

"Lengo ni kutafuta njia ambayo inaheshimu sheria za kimataifa vilevile kuheshimu mamlaka ya nchi ya Denmark na Greenland," ameongeza.

Waziri Mkuu wa Greenland Jens-Frederik Nielsen (kushoto, kwenye theluji) akionekana kwenye maandamano ya kupinga maneno na vitendo vya Marekani  juu ya udhibiti wa Greenland huko Nuuk, mji mkuu wa Greenland, eneo linalojitawala la Denmark, Januari 17, 2026. (Picha na Anders Kongshaug/Xinhua)

Frederiksen amesema kwamba NATO inaweza tu kujadiliana kwa niaba ya NATO mambo yanayohusu vitendo vyake huko Arctic. Ameongeza kuwa pande zote zilikubaliana kwamba mataifa ya Arctic yanapaswa kuimarisha ushirikiano na kudumisha uwepo wa muda mrefu katika eneo hilo.

Frederiksen pia amesisitiza mistari myekundu ya Denmark, akisema kwamba mustakabali wa Greenland unapaswa kuamuliwa na Greenland na mamlaka yake haijadiliki.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha