Lugha Nyingine
Jeshi la Somalia laua wapiganaji 130 wa al-Shabaab
(CRI Online) Januari 23, 2026
Somalia imethibitisha kwamba vikosi vyake vya usalama vimeua wapiganaji zaidi ya 130 wa al-Shabaab kufuatia mapigano makali katika eneo la kusini mwa nchi hiyo siku ya Jumatano.
Wizara ya Ulinzi ya nchi hiyo imesema jana Alhamisi kwamba vikosi maalum vya Jeshi la Somalia, vikiungwa mkono na vikosi vya usalama vya Jubaland na washirika wa kimataifa, pia vimezima shambulio katika kambi ya kijeshi kwenye kisiwa cha kimkakati cha Kuday.
Wizara hiyo pia imesema, usalama huko Kuday na maeneo ya jirani sasa uko chini ya udhibiti kamili wa Jeshi la Somalia, ambalo liko kwenye hali ya tahadhari likiendelea na operesheni za kuleta utulivu ili kuzuia vitisho vyovyote vilivyobaki.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



