Lugha Nyingine
Wanigeria zaidi ya milioni moja wako hatarini kukosa msaada wa chakula
Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP) limeonya kuwa, watu zaidi ya milioni moja kaskazini mashariki mwa Nigeria watakosa msaada wa dharura wa chakula na lishe ndani ya wiki chache kama ufadhili mpya wa fedha hautapatikana.
Katika taarifa yake iliyotolewa jana Alhamisi, WFP imemnukuu mwakilishi mkazi wa WFP nchini Nigeria David Stevenson akisema, kwa mara ya kwanza, msaada utakaotolewa nchini Nigeria utatosheleza watu 72,000 pekee kutokana na uhaba wa fedha.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Nigeria inakabiliwa na msukosuko mbaya zaidi wa njaa katika miaka ya karibuni, na watu karibu milioni 35 wanakadiriwa kukabiliwa na hali mbaya zaidi ya chakula katika msimu wa mavuno wa mwaka 2026.
Stevenson amesema, wakati huu si wa kusimamisha msaada wa chakula, kwani kufanya hivyo kutasababisha msukosuko mkubwa wa kibinadamu, usalama, na athari za kiuchumi kwa watu wengi walio hatarini ambao wamelazimika kukimbia makazi yao kutafuta chakula na hifadhi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



