Lugha Nyingine
EAC yazindua mfumo wa kwanza wa kikanda kuongeza utayari wa kukabiliana na magonjwa ya mlipuko
(CRI Online) Januari 23, 2026
Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) jana imezindua Mfumo wake wa kwanza wa Sera ya Kikanda ya Kuzuia, Utayari na Kukabiliana na Magonjwa ya Mlipuko, ili kuimarisha hatua za pamoja dhidi ya matukio ya dharura ya afya ya umma katika nchi nane wanachama wa Jumuiya hiyo.
Taarifa iliyotolewa na EAC jana Alhamisi imesema kuwa mfumo huo uliozinduliwa katika makao makuu yake mjini Arusha, Tanzania, umeidhinishwa na Bodi ya 25 ya Mawaziri wa Afya ya EAC mwezi Mei mwaka 2025.
Taarifa hiyo imesema, mfumo huo unatoa dira kwa ajili ya kuimarisha ufuatiliaji, utayari na kukabiliana na magonjwa, ukijikita zaidi katika usawa na ulinzi wa watu walio hatarini zaidi.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



