China ni mdau muhimu katika mpito wa maendeleo endelevu duniani, asema Mkuu wa WBCSD

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 23, 2026

Peter Bakker (kushoto), Rais wa Baraza la Biashara Duniani kwa Maendeleo Endelevu (WBCDS), akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari wakati wa Kongamano la Uhifadhi Duniani la Umoja wa Kimataifa wa Uhifadhi wa Mazingira (IUCN) mjini Jeju, Korea Kusini, Septemba 8, 2012. (Xinhua/Park Jin-hee)

DAVOS, Uswisi - China imeibuka kuwa mdau muhimu katika mpito wa maendeleo endelevu duniani na iko katika nafasi ya kubeba jukumu muhimu katika kipindi kinachofuata cha maendeleo endelevu, kwa mujibu wa Peter Bakker, Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Biashara Duniani kwa Maendeleo Endelevu (WBCDS).

Katika mahojiano ya maandishi na Shirika la Habari la China, Xinhua wakati wa mkutano wa mwaka wa Baraza la Uchumi Duniani (WEF) mjini Davos, Uswisi, Bakker amebainisha hatari tatu kuu zilizoikabili dunia: athari halisi za mabadiliko ya tabianchi zinazovuruga tija na uwekezaji, mgawanyiko wa kisiasa wa kijiografia unaoathiri biashara na minyororo ya thamani, na mabadiliko ya haraka ya kiteknolojia kama vile akili bandia (AI) yanayozidi uwezo wa mifumo ya usimamizi na uhimilivu wa nguvukazi kuendana nayo.

Amesema kwamba kipaumbele kwa jumuiya ya uchumi duniani ni kuoanisha mtaji, sera, na hatua za kibiashara ili kuharakisha mipito ya uchumi unaosababisha kaboni chache, kuingiza mikakati chanya kwa mazingira ya asili, na kufanya mifumo mikuu ya biashara ya mzunguko kuwa ya kawaida.

"China ni uchumi wakilishi unaopitia kwa mafanikio mchakato wa mageuzi," Bakker amesema. Amesisitiza majukumu matatu ya China: kuwa kituo kikuu cha uzalishaji wa viwanda, kuwa na mfumo wa ikolojia wa uvumbuzi unaokua kwa kasi, na kuongoza katika kupanua matumizi ya teknolojia safi, akibainisha kuwa "uwezo huu unaelekeza njia za kimataifa za kuondoa kaboni."

Picha ikionyesha wafanyakazi wa Kampuni ya Kusambaza Umeme ya Gridi ya Taifa ya Bortala wakifanya doria karibu na eneo la utalii la Ziwa Sayram ili kuhakikisha usambazaji wa umeme katika Eneo Linalojiendesha la kabila la Wamongolia la Bortalan, katika Mkoa Unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang, kaskazini magharibi mwa China, Julai 17, 2025. (Picha na Yin Tianjie/Xinhua)

Bakker amesisitiza kuongezeka kwa ushiriki wa China katika ushirikiano wa kimataifa, ikiwemo kupitia "Mazungumzo ya Maziwa Mawili," ambapo kampuni za China zinaonyesha dhamira thabiti ya kushiriki mbinu bora, kuendeleza suluhu kwa pamoja na kuunganisha uvumbuzi na masoko ya kimataifa.

Bakker ameelezea imani yake kwamba China itabeba jukumu muhimu katika kipindi kinachofuata cha maendeleo endelevu, si tu katika kutekeleza mpito wake wa ndani, bali pia katika kuwezesha utekelezaji wa kimataifa kwa kiwango kikubwa.

Akizungumzia kaulimbiu ya Baraza la Uchumi Duniani ya mwaka huu, "Moyo wa Mazungumzo," Bakker amesema, "Moyo wa mazungumzo hukosekana zaidi pale ambapo uaminifu umepungua - kati ya siasa za kijiografia na masoko, kati ya shinikizo za muda mfupi na vipaumbele vya muda mrefu, na kati ya matarajio makubwa na utekelezaji."

Picha hii iliyopigwa Januari 18, 2026 ikionyesha mandhari ya mji wa Davos, Uswisi ambako Mkutano wa mwaka wa Baraza la Uchumi Duniani (WEF) 2026 unafanyika kuanzia Januari 19 hadi 23. (Xinhua/Lian Yi)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha