Watu wawili wapoteza maisha kutokana na dhoruba kubwa ya theluji nchini Marekani

(CRI Online) Januari 26, 2026

Watu wawili wamefariki dunia kutokana na baridi kali katika Jimbo la Louisiana nchini Marekani wakati dhoruba kubwa ya theluji ilipokumba maeneo mengi nchini humo.

Dhoruba hiyo iliyoletwa na upepo kutoka aktiki na kuenea kuanzia Tambarare ya Kati na ya Kusini hadi Pwani ya Mashariki, ilianzia Ijumaa iliyopita na imetabiriwa kuendelea hadi leo Jumatatu.

Takwimu zinaonyesha kuwa watumiaji zaidi ya milioni 1 sasa wanakosa umeme, haswa katika majimbo ya Tennessee, Mississippi na Louisiana. Usafiri zaidi ya elfu 30 za ndege pia zimeathiriwa kutokana na dhoruba hiyo.

Hadi wakati habari inaripotiwa, watu takriban milioni 200 nchini humo walikuwa bado wako kwenye tahadhari ya kiwango fulani juu ya dhoruba hiyo, na idadi ya kaunti zilizo kwenye tahadhari ya dhoruba hiyo kwa wakati mmoja imevunja rekodi katika historia ya Marekani.

(Wahariri wa tovuti:Zhao Jian)

Picha