Mawaziri Wakuu wa Italia na Norway Wakosoa maneno aliyosema Trump Juu ya mhusika NATO Nchini Afghanistan

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 26, 2026

Rais wa Marekani Donald Trump (mbele) akihudhuria mkutano na waandishi wa habari kufuatia mkutano wa viongozi wa Jumuiya ya NATO mjini The Hague, Uholanzi, Juni 25, 2025.. (Xinhua/Zhao Dingzhe)

Rais wa Marekani Donald Trump (mbele) akihudhuria mkutano na waandishi wa habari kufuatia mkutano wa viongozi wa Jumuiya ya NATO mjini The Hague, Uholanzi, Juni 25, 2025.. (Xinhua/Zhao Dingzhe)

ROME - Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni na mwenzake wa Norway Jonas Gahr Store wameeleza ukosoaji juu ya maneno aliyosema Rais wa Marekani Donald Trump ambaye aliashiria kwamba vikosi vya jeshi visivyo vya Marekani vya Jumuiya ya NATO vilikuwa vimebaki nje ya mstari wa mbele wakati wa vita nchini Afghanistan.

Kwenye taarifa yake juzi Jumamosi, Meloni alikumbuka kwamba baada ya mashambulizi ya kigaidi ya Septemba 11, 2001 dhidi ya Marekani, NATO ilitumia Kifungu cha 5 kwa mara ya kwanza na ya pekee katika historia yake kwa kuchukua hatua ya kufanya mshikamano na Marekani.

"Italia iliitikia mara moja pamoja na washirika wake, ikipeleka maelfu ya wanajeshi na kuchukua wajibu kamili kwa makao makuu ya kanda ya Magharibi, ambayo ni moja ya maeneo muhimu zaidi ya operesheni ya jukumu zima la kimataifa," taarifa hiyo imesema.

Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Roma, Italia, Januari 9, 2026. (Picha na Alberto Lingria/Xinhua)

Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Roma, Italia, Januari 9, 2026. (Picha na Xinhua)

Waziri Mkuu wa Norway Jonas Gahr Store akikutana na waandishi wa habari wa kigeni mjini Oslo, Norway, Mei 19, 2025. (Xinhua/Zhang Yuliang)

Waziri Mkuu wa Norway Jonas Gahr Store akikutana na waandishi wa habari wa kigeni mjini Oslo, Norway, Mei 19, 2025. (Xinhua/Zhang Yuliang)

"Waliojitolea mihanga kwa ajili ya nchi, walionusurika na wale waliohudumu Afghanistan wanastahili kuelezewa kwa ukweli na kuheshimiwa," Store ameandika katika taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook.

"Maneno aliyosema Rais wa Marekani ni ya kutowaheshimu. Ninaelewa malalamiko makali ya wanajeshi waliostafu na jamaa zao." ameongeza.

Trump alikiambia Kipindi cha Fox Business cha Kituo cha Habari cha Televisheni cha Fox siku ya Alhamisi kwamba Marekani haikuwahi kuhitaji wanajeshi wasio wa Marekani wakati wa vita nchini Afghanistan, ambao "walikuwa wamebaki nyuma kidogo, kidogo nje ya mstari wa mbele."

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha