China yakabidhi mabaharia 17 wa Ufilipino waliookolewa kutoka kwa meli iliyozama kwa Ufilipino

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 26, 2026

Askari wa Kikosi cha Walinzi wa Pwani wa China (CCG) wakitekeleza operesheni ya uokoaji baada ya meli ya kigeni ya mizigo kupinduka katika maji ya eneo la Kisiwa cha Huangyan, kusini mwa China, Januari 23, 2026. (Walinzi wa Pwani ya China/kupitia Xinhua)

Askari wa Kikosi cha Walinzi wa Pwani wa China (CCG) wakitekeleza operesheni ya uokoaji baada ya meli ya kigeni ya mizigo kupinduka katika maji ya eneo la Kisiwa cha Huangyan, kusini mwa China, Januari 23, 2026. (Walinzi wa Pwani ya China/kupitia Xinhua)

BEIJING - China jana Jumapili ilikabidhi mabaharia 17 wa Ufilipino iliowaokoa kutoka ajali ya meli iliyopinduka karibu na Kisiwa cha Huangyan kwa Ufilipino.

Siku ya Ijumaa, meli ya mizigo iliyosajiliwa Singapore iliyokuwa ikielekea China kutoka Ufilipino ilipinduka kwenye maji karibu na Kisiwa cha Huangyan. Wawili kati ya mabaharia hao 17 waliookolewa wamethibitishwa kufariki. Wengine wanne bado hawajulikani walipo.

Saa 6:46 alfajiri ya Ijumaa, tawi la Sansha la kikosi cha utafutaji na uokoaji wa baharini lilipokea taarifa kutoka kituo cha utafutaji na uokoaji wa baharini cha Mkoa wa Hainan, ambacho kilisema meli ya mizigo iliyosajiliwa Singapore "DEVON BAY" iliyokuwa ikielekea Mkoa wa Guangdong kusini mwa China kutoka Ufilipino ilikuwa imepoteza mawasiliano kwenye maji umbali wa takribani maili 55 za baharini kaskazini magharibi mwa Kisiwa cha Huangyan cha China, ikiwa na jumla ya wafanyakazi 21 wa Ufilipino ndani yake.

Taarifa iliyotolewa na kituo hicho ilieleza kuwa, mara ya mwisho kuwasiliana na meli hiyo ilikuwa saa 3:26 usiku wa Alhamisi, wakati wafanyakazi wa meli hiyo walipotoa taarifa kwamba meli hiyo ilikuwa imeegemea kwa kiwango kikubwa na maji yalikuwa yakifurika ndani yake. Kimesema kuwa, mawasiliano yalikatika baada ya hapo wakati huohuo kiashiria cha dharura cha nafasi ya meli hiyo kisichotumia waya baadaye kilitoa ishara ya kengele.

Askari wa Kikosi cha Walinzi wa Pwani wa China (CCG) wakimwokoa mwanamabaharia wa Ufilipino baada ya meli ya kigeni ya mizigo kupinduka kwenye maji ya Kisiwa cha Huangyan, kusini mwa China, Januari 23, 2026. (Walinzi wa Pwani wa China/kupitia Xinhua)

Askari wa Kikosi cha Walinzi wa Pwani wa China (CCG) wakimwokoa mwanamabaharia wa Ufilipino baada ya meli ya kigeni ya mizigo kupinduka kwenye maji ya Kisiwa cha Huangyan, kusini mwa China, Januari 23, 2026. (Walinzi wa Pwani wa China/kupitia Xinhua)

Baada ya kupokea taarifa hiyo, tawi hilo la utafutaji na uokoaji wa baharini la Sansha lilianzisha mara moja operesheni ya kimataifa ya uokoaji iliyohusisha mashirika mbalimbali.

Kamandi ya Kivita ya Kusini ya Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA) ilituma ndege za kijeshi kufanya shughuli za utafutaji juu ya maji kwenye eneo la ajali hiyo.

Meli mbili za karibu za Walinzi wa Pwani wa China (CCG) pia zilijiunga na operesheni hiyo ya uokoaji, sambamba na timu kutoka Ofisi ya Uokoaji ya Nanhai ya Wizara ya Uchukuzi ya China.

Meli mbalimbali za kibiashara za kimataifa, zikiwemo meli zilizosajiliwa nchini Liberia, Panama, na Japani, pia zilijiunga na operesheni hiyo ya utafutaji.

Kwa ombi la Ufilipino, CCG saa 8:43 mchana jumapili ilikabidhi kwa mafanikio mabaharia waliookolewa kwa Walinzi wa Pwani wa Ufilipino kwenye maji ambako ajali hiyo ilitokea.

“Baada ya ajali hiyo ya meli, CCG ilituma mara moja meli kufanya operesheni za uokoaji wa kibinadamu kwa mabaharia waliokuwa hatarini, na itaendelea kuhamasisha vikosi husika kwa juhudi za utafutaji na uokoaji,” CCG imesema.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha