Lugha Nyingine
Kaimu rais wa Venezuela asema tofauti na Marekani zitatatuliwa kwa njia ya diplomasia
(CRI Online) Januari 26, 2026
Kaimu Rais wa Venezuela Bibi Delcy Rodriguez amesema tofauti kati ya Venezuela na Marekani zitatatuliwa kwa njia za kidiplomasia.
Akizungumza jana Jumapili katika hafla na wafanyakazi kwenye kiwanda cha kusafisha mafuta cha Puerto La Cruz kaskazini mashariki mwa Venezuela, Rodriguez amesema serikali yake itashughulikia migogoro ya muda mrefu na Marekani ana kwa ana kupitia kile alichokielezea kuwa diplomasia ya Bolivarian.
Amesema Venezuela haikuwahi kufikiria kwamba mji mkuu wake wa Caracas ungeshambuliwa na taifa la kigeni, akirejelea tukio la tarehe 3 mwezi huu, wakati vikosi vya Marekani vilipoishambulia Caracas na kumteka kwa nguvu Rais Nicolas Maduro na mkewe.
(Wahariri wa tovuti:Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



