Ethiopia yatangaza kumalizika kwa mlipuko wa ugonjwa wa Marburg

(CRI Online) Januari 27, 2026

Wizara ya Afya ya Ethiopia imetangaza kumalizika kwa mlipuko wa ugonjwa wa Marburg nchini humo.

Akihutubia hafla moja jana Jumatatu mjini Addis Ababa, waziri wa afya wa Ethiopia Mekdes Daba amesema kutokana na kutokuwa na mtu aliyeambukizwa kwa siku 42 mfululizo, nchi hiyo sasa haina virusi hivyo kulingana na vigezo vilivyowekwa na Shirika la Afya Duniani.

Ameielezea hatua hiyo muhimu katika kudhibiti mlipuko huo kuwa ni "mafanikio makubwa katika historia ya mfumo wa afya wa nchi hiyo."

Wakati huo huo, serikali ya Ethiopia imetoa salamu za rambirambi kwa familia za waliopoteza maisha kutokana na virusi hivyo.

(Wahariri wa tovuti:Zhao Jian)

Picha