Timu ya madaktari ya China yaleta kliniki ya bila malipo kwa watoto yatima wa Zanzibar, Tanzania

(CRI Online) Januari 27, 2026

Madaktari kutoka Kundi la 35 la Timu ya madaktari wa China visiwani Zanzibar, Tanzania wakifanya kliniki ya bila malipo kwa watoto yatima wenyeji huko Zanzibar, Tanzania, Januari 25, 2026. (Kundi la 35 la Timu ya madaktari wa China visiwani Zanzibar/kupitia Xinhua

Madaktari kutoka Kundi la 35 la Timu ya madaktari wa China visiwani Zanzibar, Tanzania wakifanya kliniki ya bila malipo kwa watoto yatima wenyeji huko Zanzibar, Tanzania, Januari 25, 2026. (Kundi la 35 la Timu ya madaktari wa China visiwani Zanzibar/kupitia Xinhua

Kundi la 35 la Timu ya Madaktari wa China visiwani Zanzibar, Tanzania imeanzisha kliniki ya bila malipo kwenye nyumba ya watoto yatima, ikiwa ni sehemu ya mpango wa huduma za matibabu bila malipo wa “Timu 100 za Madaktari katika Vijiji 1000”.

Shughuli hiyo iliyofanyika Ijumaa, mwishoni mwa wiki iliyopita ilitoa huduma za matibabu bila malipo kwa watoto wapatao 70 kwenye vitengo vinane, ikiwemo Tiba ya Jadi ya Kichina na upasuaji.

Ili kukidhi mahitaji ya afya ya watoto hao yatima, timu hiyo pia iliandaa semina ya elimu ya afya. Ikitumia vipeperushi vya Kiswahili, madaktari wa timu hiyo waliwafundisha watoto kuhusu jinsi ya kuzuia magonjwa, kujisafisha kwa njia za kisayansi na kutunza meno.

Katika shughuli hiyo, timu hiyo pia ilichangia vitu vya mahitaji, ikiwa ni pamoja na dawa, vifaa vya kujifunzia na chakula.

Mkuu wa timu hiyo, Bao Zengtao amesema watoto wanabeba mustakabali wa urafiki kati ya China na Afrika, na timu yake inalenga kuhimiza mabadilishano na ushirikiano wa kina kwa kuitikia wito wa Mwaka 2026 wa Mabadilishano ya kati ya Watu na Watu wa China na Afrika.

(Wahariri wa tovuti:Zhao Jian)

Picha